Viwakilishi ni aina ya maneno yanayosimamia nomino katika mikadha mbalimbali. Ijapokuwa viwakilishi husimania nomino, haina maana kwamba nomino inayowakilishwa huwa haipo kila mara.
MAANA YA MISIMU
Misimu ni semi ndogo ndogo za mpito zinazotumiwa katika mazingira fulani kisha kufifia baada ya mazingira yale kutoweka. Aidha, semi za misimu hujitokeza kama tamathali za usemi na zinatofautiana kimaeneo.
UTUNGO: KUANDIKA RESIPE
Katika upishi wa kisasa na wa kitaalamu, kuna maagizo au maelezo fulani mahsusi yanayoambishwa mapishi. Maagizo na maelezo haya hujulikana kitaalamu kama resipe.
Maana ya mafumbo
Mafumbo ni semi ambazo maana yake imejificha na inabidi kufumbuliwa. Mafumbo ni ya aina mbili: vitendawili na mizungu. Vitendawili ni semi fupifupi za fumbo zinazotumia picha, tamathali na ishara kueleza wazo lililofichika ambalo ndilo jawabu la fumbo.
SARUFI – VIWAKILISHI: VIONYESHI, VIMILIKISHI, VIULIZI, VIREJESHI, A-UNGANIFU
Viwakilishi ni aina ya maneno katika sarufi ya lugha yenye uamilifu wa kusimamia nomino kwenye miktadha mbalimbali.
UTUNGO: WASIFU
Wasifu ni maelezo kuhusu jinsi mtu, kitu au mahali panavyoonekana. Wasifu wa mtu, kwa mfano, unajumlisha sifa za maisha yake, maumbile na pengine tabia zake. Mara nyingi, sifa zinazosisitizwa ni mchango wa mtu katika tukio la kijamii kama vile siasa, uchumi, usomi, n.k.
FASIHI: NGOMEZI
Ngomezi ni aina ya fasihi simulizi inayoshughulisha ngoma. Kwa karne nyingi, jamii za Kiafrika zilitumia ngoma kupitishia ujumbe fulani mahsusi.
SARUFI: MNYAMBULIKO WA VITENZI: VITENZI VYA SILABI MOJA
Katika vitenzi vya silabi moja, inabidi ku iongezwe ili neno litamkike kwa msingi uliotajwa hapo juu.
UTUNGO: MIALIKO
Mwaliko ni aina ya maandishi mafupi mithili ya barua rasmi, yanayoandikwa na mtu au kundi la watu kwa lengo la kuwakaribisha wenzao katika hafla au dhifa fulani mahsusi.
SARUFI: MNYAMBULIKO WA VITENZI VYENYE ASILI YA KIGENI
Katika kunyambua vitenzi vyenye asili ya kigeni, kiambishi huambikwa kwenye mwisho wa kitenzi. Irabu ya mwisho inaweza kudondoshwa au kuunganishwa na ya kiambishi.