TAWASIFU NA WASIFU

Katika utunzi wa kisanaa, kuna kitengo kinachohusiana na utoaji sifa za mtu au watu. Sifa za mtu zinaweza kutolewa na mtu mwenyewe (yaani, mwandishi) au na mtu mwingine.

UTUNGO: WASIFU

Wasifu ni maelezo kuhusu jinsi mtu, kitu au mahali panavyoonekana. Wasifu wa mtu, kwa mfano, unajumlisha sifa za maisha yake, maumbile na pengine tabia zake. Mara nyingi, sifa zinazosisitizwa ni mchango wa mtu katika tukio la kijamii kama vile siasa, uchumi, usomi, n.k.