MUKHTASARI NI NINI?

Muhtasari au ufupisho ni mbinu muhimu sana katika taaluma ya uandishi. Ni uwezo wa kueleza maana iliyomo katika habari kwa kutumia idadi chache ya maneno, bila kupotosha maana ya makala asilia.

SARUFI: UAKIFISHAJI

Uakifishaji ni ustadi wa kutumia herufi na alama za uandishi katika kuyapa maandishi maana bainifu zaidi. Uakifishaji hurahisisha mawasiliano kwa kumwelekeza mwandishi na msomaji ipasavyo.

SEMI ZA KISWAHILI

Semi ni maneno yanayosema vitu kwa njia fiche. Ni njia mojawapo ya kufumba kile kinachosemwa.

AINA ZA INSHA

Insha ni mtungo wa maneno yaliyoandikwa kwa lugha ya nathari au mchezo wa kuigiza (drama).

FASIHI: UMUHIMU WA FASIHI SIMULIZI

Fasihi simulizi ni fasihi iliyo kongwe zaidi kwa sababu iliibuka pale binadamu alipounda lugha kama chombo cha mawasiliano

SAJILI: MATANGAZO

Sajili ni matumizi ya lugha katika mazingira na viwango maalum. Baadhi ya viwango hivi ni kama vile dini, sheria, biashara, michezo na magazeti. Sajili pia hujulikana kama rejesta.

SARUFI: UKANUSHAJI WA NYAKATI NA HALI

Ukanushaji ni hali ya kukataa au kutokubaliana na kauli fulani. Ni kusema sivyo, na ni kinyume cha kukubali au uyakinisho.

METHALI ZA KISWAHILI

Methali ni kifungu cha maneno yenye hekima yanayotumiwa kimafumbo katika kuwaelekeza wanadamu. Methali zimejikita katika mila, desturi, mazingira na kazi za wanajamii.

UANDISHI WA INSHA

Insha ni mtungo wa maneno yaliyoandikwa kwa mtindo wa nathari (tutumbi) au tamthilia (natiki) juu ya jambo mahsusi.

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA KAZI ZA SANAA

Tamathali za usemi ni mtindo wa kutumia lugha kwa ustadi kwa makusudi ya kupamba kazi ya sanaa. Aidha, fungu la maneno huteuliwa na kutumiwa na mwandishi kwa lengo la “kufananisha” kinachoelezwa na hali au kitu fulani maishani.