MAHOJIANO NA DAYALOJIA

Dayalojia ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi. Dayalojia inaweza kuwasilishwa kimazungumzo au kimaandishi.

UUNDAJI WA NOMINO KUTOKANA NA VITENZI: KIGENI, KUAMBISHA VIAMBISHI

(a) Vitenzi vya kigeni Katika Sarufi ya Kiswahili, kuna vitenzi vya kigeni ambavyo hutumiwa katika uundaji wa nomino. Kwa mfano: Kitenzi cha Kigeni Nomino Inayovyazwa Fahamu Ufahamu Safiri Safari, Msafiri, Usafiri Sahau Usahaulivu Samehe Usamehevu, Msamaha, Msamehevu Afiki (Ma)afikiano Ahidi Ahadi (b) Vitenzi vya kuambisha viambishi Nomino mbalimbali huundwa kwa …

MALUMBANO YA UTANI

Malumbano ya utani ni utanzu wa vichekesho katika fasihi simulizi. Jamii za Kiafrika zina tafrija mbalimbali zinazojumuisha furaha na vichekesho nyingi kama njia mojawapo ya burudani miongoni mwa wanajamii. Lakini katika vichekesho hivyo kuna mafunzo tele.

KUMBUKUMBU ZA MKUTANO

Kumbukumbu za mkutano ni hifadhi au rekodi ya utaratibu wa mkutano. Hii ni mojawapo ya maandishi maalum yenye utaratibu au kaida zinazokubalika kimataifa. Mikutano hujadili mambo mengi ambayo hayana budi kuhifadhiwa

SARUFI -VIELEZI: IDADI, KIASI, MAHALI

Kielezi ni neno linalotumiwa kueleza zaidi juu ya kitenzi, kivumishi ama kitenzi kingine. Somo hili linashughulikia vielezi vya idadi, kiasi na mahali.

MAANA YA MAWAIDHA

Mawaidha ni ada za waja zinazosisitiza utubora au mwenendo mzuri katika maisha. Aidha, ni maneno mazuri ya maonyo, makanyo au mafunzo yanayotoa mwongozo au usia.

KUANDIKA RIPOTI

Ripoti ni habari iliyotayarishwa na mtu au watu ili kusomwa baadaye. Kuna aina mbili za ripoti: ripoti ya kawaida na ripoti maalum.

FASIHI SIMULIZI: NYIMBO, SIFA, AINA

Nyimbo ni tungo zenye mahadhi. Mawimbi ya mahadhi au sauti hizo hupanda na kushuka kutegemea wimbo unaotongolewa.

SARUFI – VIELEZI: NAMNA, WAKATI

Kielezi ni neno linalotumiwa ili kuelezea zaidi juu ya kitenzi, kivumishi au kitenzi kingine. Mifano ya vielezi ni: sana, kabisa, mno, zaidi.

KUANDIKA TAHARIRI

Tahariri ni taarifa inayochambua mada mahsusi kwa kina. Aidha, huandikwa kwa lugha ya ushawishi na huzingatia mada. Lengo huwa ni kumfanya mtu abadilishe msimamo wake kuhusu jambo fulani. Lugha yake imechujwa na aya ni fupifupi.