SARUFI – MUUNDO WA SENTENSI: KIKUNDI NOMINO, KIKUNDI TENZI

Kila lugha ina muundo wake wa sentensi. Muundo huu unaongozwa na sheria zinazofafanua namna maneno mbalimbali yatakavyohusiana. Kwa jumla sentensi huwa na nomino na kitenzi, pamoja na aina nyingine za maneno.

SARUFI: SENTENSI ZA KISWAHILI

Sentensi ni mwambatano wa maneno wenye maana. Usahihi wa mwambatano huo hutegemea sheria za lugha inayohusika. Maneno kwenye sentensi huwa katika mafungu yenye uhusiano wa kimuundo na kimatumizi.

INSHA YA KITAALUMA

Insha ya kitaaluma inatakikana iwe dhahiri, iliyolenga mada inayoshughulikiwa na rahisi kufahamika. Insha ya aina hii inapaswa kuwa na mtiririko wenye mantiki.

HADITHI FUPI: KIPENDACHO MOYO NI DAWA

Wasitara hasumbuki, wa mbili havai moja Kidawa. Baba na mama hawakukutakia heri pale walipotaka kukuoza Dau, mwanamume mkofu, mchafu, hakika hakukustahilia. Lo, yasini! Si Kidawa wewe. Unajiona leo ulivyotononoka? Dunia yote ni yako. Moyo maluuni wa Kidawa ulimpa nguvu kwelikweli. Unajua kwa nini Kidawa akahisi hivyo? Ngoja nikueleze basi. Alikuwa …

UTUNGO: KUANDIKA NA KUJAZA HOJAJI

Hojaji ni mkusanyiko wa maswali ambayo hutumiwa kama kifaa katika kazi ya utafiti. Maswali haya hayatungwi kiholela bali hujifunga sana na mada na aina ya utafiti wa nyanjani unaohusika.

SARUFI: UPATANISHO WA KISARUFI: VIREJESHI ‘O’ NA ‘AMBA-

Virejeshi ni viambishi vinavyorejesha nomino kwa kitendo. Aidha, hutokea kabla au baada ya mzizi wa kitenzi ili kurejelea nomino ambayo habari yake inatolewa.

KUANDIKA: KUJAZA FOMU

Fomu ni aina ya maandishi yenye maagizo fulani na mapengo yanayohitaji kujazwa kwa ufupi na usahihi.

SARUFI – NGELI ZA NOMINO: UPATANISHO WA KISARUFI NA VIVUMISHI VYA A-UNGANIFU

Lugha ya Kiswahili, kama lugha nyingine za Kibantu, ina utaratibu wa nomino ambapo muundo wa viambishi vya maneno (vitenzi, vivumishi, viwakilishi, vielezi na kadhalika) huongozwa na aina ya nomino.

SARUFI – MWINGILIANO WA MANENO: KIVUMISHI/KIWAKILISHI

Kufikia sasa, mmesoma vitabu mbalimbali vyenye maelezo tofauti kuhusu vivumishi na viwakilishi. Katika baadhi ya vitabu vya Sarufi ya Kiswahili, kumekuwa na tatizo la maneno mengine kuainishwa kama vivumishi ilhali yangefaa kuainishwa kama viwakilishi. Kwa mfano, katika kitabu cha Kapinga (1983) kiitwacho Sarufi Maumbo ya Kiswahili, mwandishi ameorodhesha aina hizi …