UTUNGO: MIALIKO

Maana ya mwaliko

Mwaliko ni aina ya maandishi mafupi mithili ya barua rasmi, yanayoandikwa na mtu au kundi la watu kwa lengo la kuwakaribisha wenzao katika hafla au dhifa fulani mahsusi. Mialiko ni njia iliyostaarabika ya kuwasiliana na umma (zamani, nafasi hii ilichukuliwa na ngoma au jaliko la wajumbe). Kuna mialiko rasmi na isiyo rasmi.

Aina za Mialiko

  • mwaliko wa arusi
  • mwaliko wa sherehe ya ushindi wa kikundi fulani katika mashindano mahsusi.
  • mwaliko wa sherehe ya kitaifa kama vile Jamhuri, Siku ya Mashujaa, kuadhimisha uzindushi wa Ukimwi, na kadhalika.

Kaida za Mialiko

Mialiko hujikita katka mambo yafuatayo:

  • ujumbe mfupi unaolenga mada kamili; kwa mfano, sentensi moja au mbili hivi.
  • lugha sahali hutumiwa.
  • uandishi “kavu” usiojumuisha mapambo ya lugha.
  • mara nyingi, mwaliko huchorwa kwenye kisanduku fulani cha karatasi chenye ruwaza inayovutia.
  • anwani, tarehe na nambari ya simu ya mwandishi/waandishi huonekana mwisho wa mwaliko wenyewe.

Mfano wa Mwaliko:

Chama cha Vijana cha Getembe

(CHAVIGE)

Mwenyekiti wa Chama cha Vijana cha Getembe, Kisii, anayo furaha tele kukukaribisha Bi. Anne Mokeira katika warsha itakayofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Busara kuanzia tarehe 14-12-2004 saa 2.00 asubuhi ili kuzungumzia athari za ukeketaji wasichana katika jamii yetu. Tunakutegemea sana kwa maoni yako ya kimaendeleo.

Ikiwa hutahudhuria binafsi tuma maoni kwa:

Moseti Mogaka

S.L.P.43896 Simu:

Kisii 0783 884 944

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *