UTUNGO: MATANGAZO

Kuna matangazo ya aina nyingi: matangazo ya biashara, vifo, ajira, harusi, michezo na kadhalika. Matangazo yana kaida zake. Kwa mfano, sharti yabainishe:

  • mtangazaji
  • tarehe ya tangazo
  • ujumbe unaowasilishwa
  • anayetarajiwa kufikiwa na ujumbe (kama sio umma kwa jumla)
  • tarehe ya mwisho ya tangazo (kama kwa mfano ni tangazo la ajira).

Lugha ya matangazo ni ya mkato na hulenga ujumbe uliokusudiwa. Ikiwa ni matangazo kwenye mabango, kama vile matangazo ya biashara, picha hutumiwa na herufi ni kubwa zaidi.

Zingatia mfano ufuatao.

TANGAZO LA BIASHARA

Kijana: Napata maumivu makali sana wakati wa kujisaidia haja ndogo na mwishowe natokwa na usaha.

Daktari: Una miaka mingapi?

Kijana: Kumi na saba.

Daktari: Labda una ugonjwa wa zinaa.

                Je, umefanya mapenzi hivi karibuni?

Kijana: (Kwa haya) Ndio, daktari.

Daktari: Ni hatari sana kufanya ngono kabla ya ndoa. Unaweza kuambukizwa kisonono, kaswende au UKIMWI. Jiepushe na tabia inayoweza kuhatarisha maisha yako! (Muziki).

Kauli mbiu: Vijana wana haki ya kufunzwa maadili mema yanayohusu afya yao!

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *