Hojaji ni mkusanyiko wa maswali ambayo hutumiwa kama kifaa katika kazi ya utafiti. Maswali haya hayatungwi kiholela bali hujifunga sana na mada na aina ya utafiti wa nyanjani unaohusika. Hojaji ni njia mojawapo ya mhoji kutambua maoni au msimamo wa mhojiwa (wahojiwa).
Mifano ya Utafiti
Shughuli za utafiti ni nyingi; baadhi yazo ni kutaka kujua:
- ikiwa bidhaa fulani inapendwa na watu wengi.
- athari ya ugonjwa miongoni mwa wanajamii wa eneo fulani.
- uhalifu katika eneo fulani mahsusi.
- sababu za kudidimia kwa tamaduni.
Aina za Maswali na Kauli za Hojaji
(i) Maswali ya mjadala
Huhitaji maelezo kidogo kutoka kwa mhojiwa ili maoni yake yabainike wazi.
(i) Maswali yaliyodhibitiwa
Haya huhitaji majibu ya aina fulani pekee; yaani, mkondo wa fikra za mhojiwa tayari umeelekezwa kwenye njia fulani. Pia, kuna maswali ya kukubali au kukataa kauli fulani.
(i) Kauli za kutathminiwa
Kauli hizi huhitaji uamuzi unaokadiria wazo au hoja kama vile: nzuri sana, nzuri kiasi, mbaya, mbaya sana na isiyofaa.
MFANO WA HOJAJI
HOJAJI KUHUSU UMASKINI VIJIJINI
Jina …………………………………………..
Jinsia …………………………………………
(Mke/Mume)……………………………..
Makazi (Mtaa au Kijiji)……………………………………………..
Idadi ya Watoto katika familia……………………………………………….
Kazi yako………………………………………………………………………………
Mapato kwa Mwaka
- : Chini ya Ksh. 20,000 [ ]
- : Baina ya Ksh. 20,000 na Ksh. 40,000 [ ]
- : Baina ya Ksh. 40,000 na Ksh. 60,000 [ ]
- : Baina ya Ksh. 60,000 na Ksh. 80,000 [ ]
- : Zaidi ya Ksh. 80,000 [ ]
Lishe
- Mnakula chakula mara ngapi kwa siku? …………………………………………..
- Chakula kilichotamalaki………………………………………………
Mavazi/Mapambo
- Una nguo ngapi za kubadilisha?………………………………………..
- Kila mtoto ana nguo ngapi?……………………………………………
- Unajinunulia nguo mara ngapi kwa mwaka?………………………………………
- Mnatumia mafuta gani kujipaka hapa nyumbani?………………………………………..
- Mnatumia sabuni gani kuoga?………………………………………………………….
- Una viatu jozi ngapi?…………………………………………………………….
- Je, kila mtoto ana viatu?……………………………………………………………
Mastakimu
- Nyumba/Shamba hili ni lako? (Ndio/La)…………………………………………….
- Unalipa kodi kiasi gani?………………………………………………………..
- Je, kuna hospitali na shule hapa karibu? …………………………………
- Je, watoto wako wote wamepata chanjo zote za utotoni?……………………………………
- Pendekeza maendeleo ambayo ungependa kuyaona hapa mtaani/kijijini……………………………………