Katika uandishi wa barua rasmi au za kikazi ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:
- Anwani ya mwandishi na tarehe.
- Anwani ya mwandikiwa. Hii iwe kushoto chini ya anwani ya mwandishi. Anwani hii iwe wima.
- Mwanzo wa barua uzingatie uhusiano wa kikazi wa mwandishi na mwandikiwa.
- Mada inayohusika.
- Barua iwe fupi yenye taarifa zilizo za lazima tu.
- Mwisho uzingatie uhusiano wa kikazi wa mwandishi na mwandikiwa.
Mifano ya Barua Rasmi
Mfano (a)
Chuo cha uhandisi,
S.L.P. 451071,
MARALAL.
Desemba 20, 2003.
Mkurugenzi,
Taasisi ya Maendeleo,
S.L.P.30167,
NAIROBI
Mkurugenzi,
KUHUSU: VITABU VYA UHANDISI
Rejelea mada iliyopo hapo juu. Tafadhali nitumie vitabu kuhusu uhandisi ambavyo mmevichapisha hivi majuzi ili tuvitathmini kwa minajili ya kuvitumia kufundishia.
Huduma ya haraka itatufanikisha.
Ndimi mwaminifu,
(Saini)
Eda Cheruto
Mkurugenzi
Mfano (b)
Kijiji cha Gede,
S.L.P. 505,
KALOLENI.
Juni 27, 2003
Afisa Masoko,
Shirika la Kilimo,
S.L.P.1567,
THIKA.
Afisa Masoko,
MINTARAFU: VIFAA VYA KILIMO
Asante sana kwa barua yako nambari KG/3/51/03 ya tarehe 30.04.2003 kuhusu bei ya vifaa vya kilimo.
Tafadhali tuletee kwa njia ya posta vifaa hivi:
VIFAA | IDADI | BEI |
Majembe | 5 @ 40/= | 200.00 |
Reki | 30 @ 40/= | 1200.00 |
Mapanga | 100 @ 50/= | 5000.00 |
Plau | 10 @ 100/= | 1000.00 |
Jumla | 7400.00 |
Pokea hundi nambari 76149 ya tarehe 27 Juni, 2003 yenye thamani ya shilingi
8000.00 (elfu nane tu) zikiwa ni pamoja na gharama za posta.
Wako, (Saini)
Lokirito Ngilu
Mwenyekiti
Tanbihi: Kumbuka kwamba ni muhimu kupigia mstari mada ya barua rasmi. Pia, mrejeshe msomaji kwenye mada