UTUNGO: BARUA KWA MHARIRI

Barua kwa mhariri inatakiwa kufuata mtindo wa barua rasmi. Zingatia:

  • anwani yako na tarehe
  • anwani ya anayepelekewa
  • mada inayoshughulikiwa
  • lugha ya kuvutia
  • mawazo yanayotiririka
  • hitimisho
  • jina la mwandishi.

Mfano wa barua kwa mhariri:

Kijiji cha Leo Yetu,

S.L.P. 4005,

KWALE.

Novemba 5, 2003

Mhariri,

Taifa Letu,

S.L.P. 9490104-0001000,

NAIROBI.

UFISADI UMEVUKA MIPAKA

Napenda kumpongeza kwa dhati mchoraji wa kibonzo kwenye Taifa Letu ya Septemba 11, 2003. Kibonzo hicho kilisawiri ufisadi kama jitu. Kiliashiria kuwa ufisadi unapigwa vita kwa njia ya unafiki tu ili kuwavisha kilemba cha ukoka wafadhili.

Wananchi wa kawaida wanateseka kila siku kwa ajili ya ubinafsi wa watu wachache wasiotosheka. Wanafikiri kwamba wanaweza kumiliki ulimwengu!

Hivi majuzi tuliandamana ili kupinga ujengaji wa kiwanda katika uwaja wa michezo. Lakini kwa sababu ya uhusiano baina ya mwenye kiwanda na serikali iliyopo, wananchi wengi walishikwa na kupelekwa mahakamani. Ufisadi umekita mizizi katika mtaa wa Leo Yetu.

Natoa wito kwa Waziri wa Wizara Dhidi ya Ufisadi achunguze yale yanayoendelea katika afisi za serikali hapa Leo Yetu. Ni muhimu kuukabili ufisadi ana kwa ana.

Wako,

Liz Mwepesi

ZOEZI

Andika barua kwa mhariri kuhusu ubaguzi unaofanyiwa watu walemavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *