Utungo wa tahadhari hutoa maelekezo na pia huonya. Kwa mfano, mwajiri anaweza kumtahadharisha mwajiriwa anayekiuka kanuni za kazi. Katika barua hiyo ya onyo, mwajiri atataja makosa yaliyofanywa, lini yalipofanywa, na labda kitakachompata mwajiriwa asipokoma. Lugha ya barua kama hiyo ni kavu na ina ukali. Lengo la lugha inayotumika ni kutoa hisia kwa anayesoma. Kwa mfano:
Mifano ya Ilani na Onyo
Mfano wa kwanza
WIZARA YA ARDHI, MAKAO NA MAJI
S.L.P.06 7289-00200
MOMBASA
ILANI KWA UMMA
KIFUNGU CHA SHERIA YA ARDHI YA SERIKALI – IBARA YA 280
Mnamo Januari 1 2004, Serikali ilitoa notisi kwa umma kupitia vyombo vya habari kwa wanaomiliki ardhi walio na masalia ya kodi kuwataka kulipa masalia kwa muda wa siku 75, la sivyo, hatua madhubuti zitachukuliwa kutwaa ardhi na masalia ya kodi kwa mujibu wa kifungu cha 77 cha sheria ya Serikali.
Tunashukuru kwamba watu wengi wameitikia mwito wa kulipa kodi na masalia ya ardhi. Hata hivyo, tunatambua kwamba baadhi hawajalipa madeni yao. Upuuzaji huu unawafanya kupigwa faini.
Kwa hivyo, notisi inatolewa kwa wote ambao bado hawajalipa kodi kwamba zimesalia siku 30 kuanzia kutolewa kwa notisi hii kulipa kiwango cha mwaka mzima ya kodi iliyosalia pamoja na faini. La sivyo, Serikali itachukua hatua za kisheria katika mahakama kuu ili kutwaa ardhi na kiasi cha pesa kilichosalia bila kuwajulisha wapuuzaji hao.
Pia fahamu kuwa, baada ya kuisha kwa muda uliowekwa kupitia kwa notisi hii, tutachapisha magazetini majina ya watu ambao hawajalipa kodi. Baadaye, tutatoa notisi ya kutwaa ardhi kwa wote wanaohusika.
Shukuru wa ARDHI
KATIBU
Mfano wa pili
FANIKISHA MAENDELEO,
S.L.P. 66872-00800,
NAIROBI.
Novemba 15, 2003
BW.LAMKA UKOGE,
S.L.P. 53412-00200,
NAIROBI.
BW.UKOGE,
MINT: BARUA YA SIRI (ONYO LA KWANZA)
Nimepokea habari kuwa hukufika kazini mnamo Novemba 7 hadi 13, 2003 bila idhini ya msimamizi wako. Pia, nimefahamishwa kuwa huonekani kufanya kazi kwa dhati siku hizi. Unatumia wakati wako mwingi kucheza karata kwenye mtambo wa tarakilishi. Maelezo uliyotoa kuhusu tabia hii hayatoshi.
Lengo la barua hii ni kukupa onyo la kwanza kuhusu tabia yako isiyofaa.
Kwa mujibu wa sheria za kampuni ya FANIKISHA MAENDELEO kifungu FM//DHAMU/5/01, ukionywa mara tatu utapoteza kazi yako.
Ikiwa una maswali kuhusu barua hii, zungumza na msimamizi wako ili akufahamishe zaidi.
Ni mimi
BIWI WAKA MKURUGENZI
Kuna matangazo mengine yanayotolewa katika maeneo ya hadhara ili kuonya.
Kwa mfano:
