SARUFI – MWINGILIANO WA MANENO: KIVUMISHI/KIWAKILISHI

Kufikia sasa, mmesoma vitabu mbalimbali vyenye maelezo tofauti kuhusu vivumishi na viwakilishi. Katika baadhi ya vitabu vya Sarufi ya Kiswahili, kumekuwa na tatizo la maneno mengine kuainishwa kama vivumishi ilhali yangefaa kuainishwa kama viwakilishi. Kwa mfano, katika kitabu cha Kapinga (1983) kiitwacho Sarufi Maumbo ya Kiswahili, mwandishi ameorodhesha aina hizi …

SARUFI – VIWAKILISHI: SIFA, NAFSI, NGELI, PEKEE, IDADI

Viwakilishi ni aina ya maneno yanayosimamia nomino katika mikadha mbalimbali. Ijapokuwa viwakilishi husimania nomino, haina maana kwamba nomino inayowakilishwa huwa haipo kila mara.