UPATANISHO WA KISARUFI: VISISITIZI NA VIVUMISHI VYA PEKEE
SARUFI – MWINGILIANO WA MANENO: KIVUMISHI/KIWAKILISHI
Kufikia sasa, mmesoma vitabu mbalimbali vyenye maelezo tofauti kuhusu vivumishi na viwakilishi. Katika baadhi ya vitabu vya Sarufi ya Kiswahili, kumekuwa na tatizo la maneno mengine kuainishwa kama vivumishi ilhali yangefaa kuainishwa kama viwakilishi. Kwa mfano, katika kitabu cha Kapinga (1983) kiitwacho Sarufi Maumbo ya Kiswahili, mwandishi ameorodhesha aina hizi …