Tamathali ya usemi:SOGA

Soga ni tamathali ya usemi ambayo ni kitumbuizo cha lugha. Aidha, huchukua mtindo wa mchezo wa kuigiza au hadithi fupi ambapo maneno yenye ulinganifu wa vina au sauti hutumiwa kimzahamzaha kwa lengo la kuchekesha.

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA KAZI ZA SANAA

Tamathali za usemi ni mtindo wa kutumia lugha kwa ustadi kwa makusudi ya kupamba kazi ya sanaa. Aidha, fungu la maneno huteuliwa na kutumiwa na mwandishi kwa lengo la “kufananisha” kinachoelezwa na hali au kitu fulani maishani.