FASIHI SIMULIZI: NYIMBO, SIFA, AINA

Nyimbo ni tungo zenye mahadhi. Mawimbi ya mahadhi au sauti hizo hupanda na kushuka kutegemea wimbo unaotongolewa.

FASIHI: NYIMBO ZA TAARAB

Nyimbo za taarab ni kielelezo bora cha ufanisi na uamilifu wa nyimbo miongoni mwa wanajamii wa mwambao wa Afrika Mashariki. ‘Taarab’ ni neno la Kiarabu lenye maana ya ‘furaha’. Ni muziki wa kustarehesha na kuwaburudisha watu wa matabaka yote. Hupoza machofu ya umma.