SARUFI: UPATANISHO WA KISARUFI: VIREJESHI ‘O’ NA ‘AMBA-

Virejeshi ni viambishi vinavyorejesha nomino kwa kitendo. Aidha, hutokea kabla au baada ya mzizi wa kitenzi ili kurejelea nomino ambayo habari yake inatolewa.

SARUFI – NGELI ZA NOMINO: UPATANISHO WA KISARUFI NA VIVUMISHI VYA A-UNGANIFU

Lugha ya Kiswahili, kama lugha nyingine za Kibantu, ina utaratibu wa nomino ambapo muundo wa viambishi vya maneno (vitenzi, vivumishi, viwakilishi, vielezi na kadhalika) huongozwa na aina ya nomino.

Ngeli zote za kiswahili na mifano

Ngeli ni mfumo wa kisarufi katika lugha ya Kiswahili ambao hutumia viambishi awali ili kuonyesha jinsia, wingi, na hali ya nomino. Ngeli za Kiswahili, kuna ngeli ya:

Ngeli ya A-WA na mifano

Hii ni ngeli ya majina ya viumbe wenye uhai k.vwatu, wanyama, ndege, wadudu, miungu, malaikan.k Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwasauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi. Hatahivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti.