Katika vitenzi vya silabi moja, inabidi ku iongezwe ili neno litamkike kwa msingi uliotajwa hapo juu.
SARUFI: MNYAMBULIKO WA VITENZI VYENYE ASILI YA KIGENI
Katika kunyambua vitenzi vyenye asili ya kigeni, kiambishi huambikwa kwenye mwisho wa kitenzi. Irabu ya mwisho inaweza kudondoshwa au kuunganishwa na ya kiambishi.
SARUFI: MNYAMBULIKO WA VITENZI
Mnyambuliko wa vitenzi ni utaratibu wa kuunda vitenzi vipya kwa kuongeza viambishi nyambulishi kwenye maumbo ya mizizi.
Mnyambuliko wa vitenzi na mifano
Mnyambuliko wa vitenzi ni urefushaji wa vitenzi kwa kuambisha mzizi wa vitenzi kwa viambishi tamati ili kuvipa vitenzi hivyo maana lengwa na halisi.