Maji ni kiowevu kisicho na rangi wala ladha kinachopatikana kwenye mito, bahari au maziwa na wakati mwingine hutokana na mvua ambacho viumbe hunywa na watu hupikia, huogea au kufulia.
Umuhimu wa maji mwilini
Je, maji ni muhimu kwa mwili? Ndiyo! Asilimia nyingi ya mwili imetengenezwa na maji: mate, damu na seli za mwili haziwezi kufanya kazi bila maji. Je, wajua kuwa bila maji huwezi kuishi kwa zaidi ya siku chache, lakini unaweza kuishi kwa wiki kadhaa bila chakula? Hapa kuna umuhimu wa maji katika mwili.