Mafumbo ni semi ambazo maana yake imejificha na inabidi kufumbuliwa. Mafumbo ni ya aina mbili: vitendawili na mizungu. Vitendawili ni semi fupifupi za fumbo zinazotumia picha, tamathali na ishara kueleza wazo lililofichika ambalo ndilo jawabu la fumbo.