HADITHI FUPI: KIPENDACHO MOYO NI DAWA

Wasitara hasumbuki, wa mbili havai moja Kidawa. Baba na mama hawakukutakia heri pale walipotaka kukuoza Dau, mwanamume mkofu, mchafu, hakika hakukustahilia. Lo, yasini! Si Kidawa wewe. Unajiona leo ulivyotononoka? Dunia yote ni yako. Moyo maluuni wa Kidawa ulimpa nguvu kwelikweli. Unajua kwa nini Kidawa akahisi hivyo? Ngoja nikueleze basi. Alikuwa …