Wasitara hasumbuki, wa mbili havai moja Kidawa. Baba na mama hawakukutakia heri pale walipotaka kukuoza Dau, mwanamume mkofu, mchafu, hakika hakukustahilia. Lo, yasini! Si Kidawa wewe. Unajiona leo ulivyotononoka? Dunia yote ni yako. Moyo maluuni wa Kidawa ulimpa nguvu kwelikweli. Unajua kwa nini Kidawa akahisi hivyo? Ngoja nikueleze basi. Alikuwa …
Hadithi Fupi za Kiswahili
Hapa chini tumekupa hadithi fupi; hadithi ya hekaya, ya mafunzo na mahaba.
Umuhimu wa hadithi
Hadithi ni uchawi, zinaweza kuunda ulimwengu usio wa halisi, hutufanya kuwa na hisia, na maoni mablimbali. Hadithi zinaweza kutufundisha kuwa na huruma, kutufanya kucheka, kulia, kuwa na woga na kisha kutufariji kwa mwisho mzuri. Hapa tuna baadhi ya umuhimu wa haithi.