MAANA YA MAGHANI

Maghani ni kipera cha fasihi simulizi kinachojumuishwa katika fani ya ushairi-simulizi. Kughani ni kitendo cha kusema kwa njia ya mahadhi (kuimba).

FASIHI SIMULIZI: NYIMBO, SIFA, AINA

Nyimbo ni tungo zenye mahadhi. Mawimbi ya mahadhi au sauti hizo hupanda na kushuka kutegemea wimbo unaotongolewa.

FASIHI: NGOMEZI

Ngomezi ni aina ya fasihi simulizi inayoshughulisha ngoma. Kwa karne nyingi, jamii za Kiafrika zilitumia ngoma kupitishia ujumbe fulani mahsusi.

FASIHI: NYIMBO ZA TAARAB

Nyimbo za taarab ni kielelezo bora cha ufanisi na uamilifu wa nyimbo miongoni mwa wanajamii wa mwambao wa Afrika Mashariki. ‘Taarab’ ni neno la Kiarabu lenye maana ya ‘furaha’. Ni muziki wa kustarehesha na kuwaburudisha watu wa matabaka yote. Hupoza machofu ya umma.

FASIHI: UAINISHAJI WA FASIHI SIMULIZI

Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha inayohifadhiwa kwa njia ya mapokezano. Ilitangulia fasihi andishi na inajishughulisha na maisha ya binadamu pamoja na mazingira yake.

Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha au maneno katika sura mbalimbali kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu. Hizi hapa ni tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi.