Aina za nomino na mifano yake

Nomino ni aina ya neno inayotaja jina la mtu, mahali, kitu, au wazo.
Aina za Nomino
Nomino za pekee/maalumu /mahususi
Nomino za kawaida
Nomino za makundi/jamii
Nomino za wingi/Fungamano
Nominoambata
Nomino za kitenzijina
Nomino dhahania.

Tofauti kati ya nomino za pekee na nomino za kawaida

Nomino za pekee ni maneno yanayotaja majina mahususi ya watu, mahali, au vitu ambavyo vina sifa ya pekee. Nomino za pekee huanza kwa herufi kubwa. Nomino hizi hutaja vitu kwa kawaida. Nomino hizi hurejelea dhana ,vitu  au viumbe vinavyopatikana duniani.