SEMI ZA KISWAHILI

Kuna maneno ya kawaida ambayo yakitumiwa katika muktadha (au mazingira) fulani hutoa maana nyingine iliyosetirika. Kwa mfano, tukisema kuwa Wario ana mkono mrefu tuna maana kwamba Wario ni mwizi. Na tukisema kuwa Wario ana mkono wazi tuna maana kwamba Wario ni mkarimu.

Semi ni maneno yanayosema vitu kwa njia fiche. Ni njia mojawapo ya kufumba kile kinachosemwa.

Sentensi zifuatazo zinaeleza mambo kimafumbo. Zifumbue.

(i) Serikali mpya ya wananchi imepiga marufuku mtindo wa kuzunguka mbuyu mtu anapotafuta huduma katika ofisi za umma.

(ii) Bwana Issa alipofika ugenini alificha kucha kwa hofu ya kubukuliwa na wenyeji wake.

(iii) Usimwamini Bi. Mwongera, ana ndimi mbili.

(iv) Majambazi wa Kariakor wamesalimu amri baada ya tangazo la msamaha la Rais.

(v) Wanasiasa wanapenda kutia chumvi maneno yao ili kuteka hisia za raia.

ZOEZI

(a) Tumia semi zifuatazo katika sentensi ili kudhihirisha maana.

(i) toa mleli

(ii) kumwita mtu chemba

(iii) hana maua

(iv) pigwa kabali

(v) kukosa kaa na gamba lake.

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *