Virejeshi ni viambishi vinavyorejesha nomino kwa kitendo. Aidha, hutokea kabla au baada ya mzizi wa kitenzi ili kurejelea nomino ambayo habari yake inatolewa. Virejeshi huweza kutokea pia kwenye mzizi “amba-“.
Tazama jedwali lifuatalo:
Ngeli | Nomino | Virejeshi |
A | Mwalimu | ambaye/aliyekuja ni Mchina. |
WA | Walimu | ambao/waliokuja ni Wachina. |
U | Mti | ambao/utakaopandwa ni mvule. |
I | Miti | ambayo/itakayopandwa ni mivule. |
KI | Chakula | ambacho/kitakachosazwa kitatupwa. |
VI | Vyakula | ambavyo/vitakavyosazwa vitatupwa. |
LI | Yai | ambalo/lililovunjika linanuka. |
YA | Mayai | ambayo/yaliyovunjika yananuka. |
I | Barua | ambayo/uliyoniandikia iliniudhi. |
ZI | Barua | ambazo/mlizotuandikia zilituudhi. |
U | Uamuzi | ambao/uliofanywa unaridhisha. |
YA | Maamuzi | ambayo/yaliyofanywa yanaridhisha. |
KU | Kucheza | ambako/walikocheza kulifurahisha. |
PA | Pahali | ambapo/nilipotengewa panatosha. |
KU | Kwahali | ambako/kulikochafuka kutasafishwa. |
MU | Mwahali | ambamo/mnamonuka mtapulizwa marashi. |