SARUFI: UKANUSHAJI WA NYAKATI NA HALI

Ukanushaji ni hali ya kukataa au kutokubaliana na kauli fulani. Ni kusema sivyo, na ni kinyume cha kukubali au uyakinisho.

Kwa mfano:

Makau anapenda mazungumzo (kuyakinisha). – Makau hapendi mazungumzo (kukanusha).

Farida ni mwimbaji mashuhuri (kuyakinisha). – Farida si mwimbaji mashuhuri (kukanusha).

Ukanushaji hubadilika kulingana na nyakati na hali mbalimbali.

Tazama sentensi zifuatazo.

(a)

(i) Nilizungumza na mwenyekiti sebuleni mwake.

(ii)Sikuzungumza na mwenyekiti sebuleni mwake.

(b)

(i) Mimi ninaenda sokoni.

(ii) Mimi siendi Sokoni.

(c)

(i) Yeye atafukuza wanafunzi.

(ii) Yeye hatafukuza wanafunzi.

(d)

(i) Nimemwona Saidi akimsaidia mhasiriwa wa Ukimwi.

(ii) Sijamwona Saidi akimsaidia mhasiriwa wa Ukimwi.

Katika kila jozi ya sentensi, sentensi ya kwanza ni uyakinisho ambapo ya pili ni ukanusho. Kutokana na miundo ya sentensi hizo, tunaweza kuona sentensi za uyakinisho na za ukanusho zikichukua herufi fulani mahsusi:

NafsiKuyakinishaKukanusha
1(Mimi) Nilimwalika nyumbani. (Sisi) Tulimwalika nyumbani.Sikumwalika nyumbani. Hatukumwalika nyumbani.
2(Wewe) Unamwalika nyumbani. (Ninyi) Mnawaalika nyumbani. (Ninyi) Mmewaalika nyumbani.Humwaliki nyumbani. Hamwaaliki nyumbani. Hamjawaalika nyumbani.
3(Yeye) Atawaalika nyumbani. (Yeye) Huenda Dubai. (Wao) Watawaalika nyumbani. (Wao) Huchoma mahindi.Hatawaalika nyumbani. Haendi Dubai. Hatawaalika nyumbani. Hawachomi mahindi.

Zingatia:

• Ukanushaji hudhihirika kwa matumizi ya kiambishi si, ha, na hu.

• Katika wakati uliopita (-li-) kiwakilishi ku huambatishwa kwenye kitenzi

kuashiria dhana ya wakati katika ukanushaji.

Kwa mfano:

Ulinikubalia – Hukunikubalia.

• Katika wakati uliopita hali timilifu (me), kiwakilishi ja huambatishwa kwenye kitenzi kuashiria dhana ya wakati katika ukanushaji. Kwa mfano:

Mmewaalika – Hamjawaalika.

Tags: 3268

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *