SARUFI – UCHANGANUZI WA SENTENSI: MSITARI, JEDWALI

Kuna njia mbalimbali za kuchanganua sentensi. Njia hizi ni:

(a) msitari

(b) jedwali

(c) mchoro wa matawi.

(a) Msitari

Katika kuchanganua sentensi kwa njia ya msitari tunaonyesha namna sentensi inavyojipambanua. Kwa mfano, ili kubainisha sehemu mbili muhimu zaidi za sentensi tunatumia kanuni ya muundo wa virai kama ifuatavyo:

S➡ KN + KT

Hii ina maana kwamba sentensi ina sehemu mbili: Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT), mathalan;

S          mtoto  ameshiba

               (KN) + (KT)

sunagnarboxenix ilawbsi

Nayo KN inaweza kujitokeza kwa namna zifuatazo:

KN          N             (yaani, KN ina Nomino)

KN          N + V      (yaani, KN ina Nomino na Kivumishi).

Nayo KT inaweza kujitokeza kwa namna zifuatazo:

KT           T

KT           T + KN

KT           T + KN + KH

Na KH inaweza kujitokeza kama:

KH          H + H + KN

Ili kuonyesha kuwa baadhi ya maneno hayo si ya lazima, tunaweza kutumia mabano. Kwa mfano;

KT           T + (KN)

Tazama kanuni zifuatazo:

S              KN + KT

KN          N + (V)

KT           T + (KN) + (KH)

KH          H + KN

Kanuni hizi zinadhihirisha kwamba kila sentensi sharti iwe na KN na KT; kwamba kila KN sharti iwe na N; kwamba kila KT sharti iwe na T; na kwamba kila KH sharti iwe na H na KN. Kutokana na kanuni hizi tunaweza kutayarisha jedwali zinazochanganua sentensi.

(b) Jedwali

Kama tulivyoona kufikia sasa, mtu anaweza kuchanganua sentensi kwa kutumia msitari, mchoro matawi au anaweza kufanya hivyo kwa kutumia jedwali. Vyovyote atakavyofanya, jambo la muhimu kuzingatia ni namna sehemu mbalimbali za sentensi zinavyohusiana kimuundo. Tunajua kwa mfano kuwa sentensi (S) ina sehemu mbili: KN na KT. Matagaa yatakayotokana na uchanganuzi yatategemea neno tawala. Ikiwa sentensi ni sentensi ambatano itakuwa na sentensi zinazoshikamanishwa na kiunganishi (U).

Kwa kutumia mfano wa Jedwali tunaweza kuchanganua sentensi kama ifuatavyo:

S
KNKT
NKVTKN
 V N
Pakamweupealimlapanya
S
U
SS
KNKTKNKT
NTNT
Mtotoamelala               na               mamaanapika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *