Uakifishaji ni ustadi wa kutumia herufi na alama za uandishi katika kuyapa maandishi maana bainifu zaidi. Uakifishaji hurahisisha mawasiliano kwa kumwelekeza mwandishi na msomaji ipasavyo. Alama nyingi za uakifishaji hukubalika mahali ambapo zimetumiwa kwa usahihi, yaani kwa maana iliyokusudiwa.
Kaida za uakifishaji:
(i) matumizi ya herufi ndogo na kubwa.
(ii) matumizi ya herufi nzito na za mlazo (italiki).
(iii) nukta na nukta pacha.
(iv) kituo.
(v) kistari kifupi na kirefu.
(vi) ritifaa.
(vii) mkwaju.
(viii) mabano au parandesi.
(ix) alama hisi.
(x) alama kiulizi.
(xi) alama za mtajo au kunukuu na kadhalika.