Kila lugha ina muundo wake wa sentensi. Muundo huu unaongozwa na sheria zinazofafanua namna maneno mbalimbali yatakavyohusiana. Kwa jumla sentensi huwa na nomino na kitenzi, pamoja na aina nyingine za maneno.
Sentensi huwa zimegawanywa katika makundi ya kiima na kiarifu, ambapo kiima husimamia kile kinachozungumziwa na kiarifu yale yanayosemwa kuhusu kitu hicho. Katika mtazamo wa kimuundo migawanyiko hii huongozwa na dhana ya neno tawala. Neno tawala katika kiima ni Nomino (N) ilhali neno tawala katika kiarifu ni Kitenzi. Kwa hivyo, sentensi (S) ina Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT).
S KN+KT
Tukitumia mchoro matawi tunapata uhusiano huu:
(a) Mwanafunzi hodari alifaulu mtihani.
S
KN KT
N V T KN V
N
Mwanafunzi hodari alifaulu mtihani mgumu
(b) Walemavu wengi wananyimwa haki.
S
KN KT
N V T KN N
Walemavu wengi wananyimwa haki
Uchanganuzi huu unaweza kufafanuliwa kwa njia ya visanduku/jedwali. Kwa jumla, tunaweza kusema kuwa muundo wa sentensi ni huu:
S KN + KT
Mstari unaonyesha “inaweza kuwa” Kundi Nomino na Kundi Tenzi kwa mpangilio huo. Muundo huu ndio:
S
KN KT
Lakini tunajua kwamba katika lugha ya Kiswahili KN inaweza kuwa na Nomino (N) na Kivumishi (V). Kwa hivyo inawezekana kuwa na uhusiano ufuatao:
KN
N V
Kijana Mzuri
Inawezekana kuwa pia na:
KN KN+KT ambapo KH ni Kundi Husishi. Tazama hapa:
KN
KN KH
N H KN
N
Kitabu cha mwanafunzi
Kama inavyoonekana hapo juu Kundi Husishi huweza kuibua Kihusishi na Kundi Nomino. Yaani:
KH H + KN
Kwa upande mwingine KT huweza kuibua Kitenzi, Kundi Nomino Husishi. Tazama hapa:
S
KN KT
N T KN
N
Baba alipika wali
KT
KH
T H KN
N
Pika wa nazi
Miundo hii sio yote inayowezekana kuwepo katika lugha ya Kiswahili. Katika somo hili, lengo limekuwa kumpa mwanafunzi fursa ya kuona namna sentensi ya Kiswahili inaweza kufafanuliwa kwa mchoro matawi. Zingatia kwamba endapo sentensi ina kiunganishi (kama “na”) sentensi hiyo itachukua muundo kama hapo chini.
Kwa mfano:
Baba alipika na mama alisoma.
S
S S
KN KT U KN KT
N T N T
Baba alipika na mama alisoma
Jambo la muhimu ni kuzingatia kuwa sentensi ya Kiswahili ina muundo unaotegemea neno tawala. Neno tawala hutoa matagaa kulingana na sheria za lugha ya Kiswahili.
Uchanganuzi huu pia unaweza kufafanuliwa kwa njia ya visanduku/jedwali.
S | ||||
KN | KT | |||
N | V | T | KN | |
N | V | |||
Mwanafunzi | hodari | alifaulu | mtihani | mgumu |