SARUFI: MNYAMBULIKO WA VITENZI: VITENZI VYA SILABI MOJA

Msingi wa vitenzi vya silabi moja umejikita katika kaida kuu ya maneno ya Kiswahili. Maneno yote ya Kiswahili yanapotamkwa, mkazo huwa katika silabi inayotangulia ya mwisho. Kwa jinsi hii, neno la Kiswahili halikamiliki bila mkazo huu.

Kwa mfano:

  • chukíza
  • barabára
  • mlíma

Katika vitenzi vya silabi moja, inabidi ku iongezwe ili neno litamkike kwa msingi uliotajwa hapo juu.

Kwa mfano:

(i) kuja

(ii) kula

(iii) kunya

(iv) kufa

(v) kupa

(vi) kunywa

Mnyambuliko

Ifuatayo ni mifano ya kutendea, na kutendewa:

KitenziTendeaTendewa
(ku)jakujiakujiwa
(ku)lakuliakuliwa
(ku)nyakunyiakunyiwa
(ku)fakufiakufiwa
(ku)pakupeakupewa
(ku)nywakunyweakunywewa

Mifano ya Sentensi:

(i) Mgeni wangu alinijia afisini.

(ii) Nilijiwa na mgeni wangu ofisini.

(iii) Nilimlia Juma chakula chake.

(iv) Mwanafunzi aliliwa chakula chake.

(v) Alinyiwa na ndege kichwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *