MAANA YA MAWAIDHA

Mawaidha ni ada za waja zinazosisitiza utubora au mwenendo mzuri katika maisha. Aidha, ni maneno mazuri ya maonyo, makanyo au mafunzo yanayotoa mwongozo au usia. Katika methali nyingi za Kiswahili pamoja na mashairi jadi, mbinu hii ya kutoa mashauri (waadhi) hujitokeza waziwazi. Pia, mawaidha hujitokeza katika nyimbo za taarab.

Tazama mifano ifuatayo:

  • Ada ya mja hunena mwungwana ni kitendo.

Yaani, mtu atagezwa kulingana na vitendo vyake wala si maneno matupu. Uungwana unatokana na vitendo vya mtu.

  • Mke hapigwi magongo, hupigwa kula na nguo.

Yaani, badala ya kumcharaza viboko mkeo, mpe chakula cha kutosha na nguo nzurinzuri. Hii ndiyo kanuni ya mume kumtunza mkewe.

  • Dunia haina wema

Dunia ina mambo mengi mabaya. Walimwengu watahiari kukufunza mambo mabaya pekee. Lengo ni kukupoteza. Lakini watasita kukufunza mambo mazuri ya kukuendeleza.

Aidha, mawaidha yanaweza kuchukua mtindo wa hotuba fupi kwa mtu (kumkanya kuhusu ulimwengu).

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *