Maana ya mafumbo

MAFUMBO

Mafumbo ni semi ambazo maana yake imejificha na inabidi kufumbuliwa. Mafumbo ni ya aina mbili: vitendawili na mizungu. Vitendawili ni semi fupifupi za fumbo zinazotumia picha, tamathali na ishara kueleza wazo lililofichika ambalo ndilo jawabu la fumbo. Mara nyingi, jibu la kitendawili ni maneno au maelezo. Kwa mfano:

(a) Shi na Shi.

Jibu: Sindano.

(b) Blanketi la baba lina chawa.

Jibu: Mbingu na nyota.

(c) Babu kazaliwa na mguu mmoja tu.

Jibu: Uyoga.

(d) Mgongo wa bibi mchafu.

Jibu: Chungu.

Mizungu ni vitendawili vitumikavyo katika hadithi kueleza dhana au wazo. Mara nyingi kauli za kimafumbo ambazo hutumiwa kwenye mizungu huonyesha ukinzani fulani wa wazo lililomo.

Kwa mfano:

Miti yote nitakwea, mtalawanda utanishinda? Yaani, nitapanda miti yote lakini ni mmoja tu utakaonishinda. Vipi?

Jibu: “Mti” huo ni ndugu wa damu moja. Si vizuri kuoa ndugu wa damu au kujuana kimwili naye.

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *