KUANDIKA RIPOTI

Ripoti ni habari iliyotayarishwa na mtu au watu ili kusomwa baadaye. Kuna aina mbili za ripoti: ripoti ya kawaida na ripoti maalum.

Ripoti ya kawaida hushughulikia mambo ya kawaida kama vile safari ya kikundi cha wanafunzi na shughuli za chama.

Ripoti maalum inahusisha tume au kikundi cha wataalamu fulani walioteuliwa kufanya uchunguzi au utafiti kuhusu suala mahsusi la kijamii. Kwa mfano, tume ya kuchunguza mfumo wa elimu, usafiri barabarani au shughuli za kiwanda.

Muundo wa Ripoti

(a) Kichwa cha habari (mada) – kiandikwe kwa herufi kubwa.

(b) Utangulizi: maelezo ya kimuhtasari kuhusu madhumuni ya ripoti.

(c) Yaliyomo:

  • mambo ambayo mwandishi aliyaona, kuanzia mwanzo, faida, hasara yake.
  • mambo haya yapewe vijichwa. Kwa mfano:

(i), (ii), (iii), (iv), (v)

(d) Hitimisho:

  • Mwandishi aonyeshe mapendekezo au msimamo wake.
  • Kisha aonyeshe ripoti imeandikwa na nani, cheo chake, na tarehe ripoti hiyo ilipoandikwa.

Mfano wa Ripoti ya Kosa la Jinai

“Niliondoka afisini mwangu katika jumba la Uaminifu saa kumi na mbili kamili. Nilipovuka barabara ya Wema nilikutana na wavulana wanne. Niliwaamkua lakini hawakunijibu. Badala yake mmoja wao alisema, “Una pesa kiasi gani?” Nilimpuuza. Ghafla mmoja akanishika kabari na kuniangusha. Wenzake walipora chochote nilichokuwa nacho. Walichukua saa yangu aina ya Seiko, viatu vyangu vyeusi, koti langu la kijivu na kibeti changu cha aina ya Gokiniwetu. Kibeti kilikuwa na kitambulisho changu cha taifa, kadi za benki, kadi ya hospitali na shilingi elfu tano taslimu. Kadi zote zilikuwa na majina yangu kamili. Wakati nikinyang’anywa mali yangu nilijaribu kupiga mayowe lakini hakuna aliyenisaidia. Watu walipita harakaharaka kwa hofu. Wezi walipomaliza kazi yao walienda. Nilipoamka nilifululiza hadi kituo cha polisi cha Utumishi na nikatoa ripoti hii. Habari nimeitoa kwa hiari.

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *