Ngomezi ni aina ya fasihi simulizi inayoshughulisha ngoma. Kwa karne nyingi, jamii za Kiafrika zilitumia ngoma kupitishia ujumbe fulani mahsusi.
UTUNGO: MIALIKO
Mwaliko ni aina ya maandishi mafupi mithili ya barua rasmi, yanayoandikwa na mtu au kundi la watu kwa lengo la kuwakaribisha wenzao katika hafla au dhifa fulani mahsusi.
Maana ya lakabu
Lakabu ni jina ambalo mtu hujipa au hupewa, mbali na jina lake halisi kutokana na umaarufu fulani au hali ya kutaniana. Lakabu huwa jina la kupanga.
FASIHI: NYIMBO ZA TAARAB
Nyimbo za taarab ni kielelezo bora cha ufanisi na uamilifu wa nyimbo miongoni mwa wanajamii wa mwambao wa Afrika Mashariki. ‘Taarab’ ni neno la Kiarabu lenye maana ya ‘furaha’. Ni muziki wa kustarehesha na kuwaburudisha watu wa matabaka yote. Hupoza machofu ya umma.
Tamathali ya usemi:SOGA
Soga ni tamathali ya usemi ambayo ni kitumbuizo cha lugha. Aidha, huchukua mtindo wa mchezo wa kuigiza au hadithi fupi ambapo maneno yenye ulinganifu wa vina au sauti hutumiwa kimzahamzaha kwa lengo la kuchekesha.
VITENDAWILI: Umuhimu wa vitendawili
Vitendawili ni kauli za mafumbo. Kauli hizi ni fupi na zina maelezo ya kuteka akili ya msikilizaji kwa lengo la kudai ufumbuzi au uteguzi.
FASIHI: UAINISHAJI WA FASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha inayohifadhiwa kwa njia ya mapokezano. Ilitangulia fasihi andishi na inajishughulisha na maisha ya binadamu pamoja na mazingira yake.