Virejeshi ni viambishi vinavyorejesha nomino kwa kitendo. Aidha, hutokea kabla au baada ya mzizi wa kitenzi ili kurejelea nomino ambayo habari yake inatolewa. Virejeshi huweza kutokea pia kwenye mzizi “amba-“.
Tazama jedwali lifuatalo:
| Ngeli | Nomino | Virejeshi |
| A | Mwalimu | ambaye/aliyekuja ni Mchina. |
| WA | Walimu | ambao/waliokuja ni Wachina. |
| U | Mti | ambao/utakaopandwa ni mvule. |
| I | Miti | ambayo/itakayopandwa ni mivule. |
| KI | Chakula | ambacho/kitakachosazwa kitatupwa. |
| VI | Vyakula | ambavyo/vitakavyosazwa vitatupwa. |
| LI | Yai | ambalo/lililovunjika linanuka. |
| YA | Mayai | ambayo/yaliyovunjika yananuka. |
| I | Barua | ambayo/uliyoniandikia iliniudhi. |
| ZI | Barua | ambazo/mlizotuandikia zilituudhi. |
| U | Uamuzi | ambao/uliofanywa unaridhisha. |
| YA | Maamuzi | ambayo/yaliyofanywa yanaridhisha. |
| KU | Kucheza | ambako/walikocheza kulifurahisha. |
| PA | Pahali | ambapo/nilipotengewa panatosha. |
| KU | Kwahali | ambako/kulikochafuka kutasafishwa. |
| MU | Mwahali | ambamo/mnamonuka mtapulizwa marashi. |